JUMLA ya watumishi wa umma 35 wa Halmashauri ya Bahi mkoani Dodoma wameondolewa kwenye ajira kutokana na kukutwa na vyeti feki katika zoezi la uhakiki huku 26 kati yao wakitoka katika sekta ya Afya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Rachel Chuwa alisema mbali na afya, sekta nyingine iliyoathirika na hali hiyo ni elimu ambayo ina watumishi nane wenye vyeti feki.
Alisema sekta ya kilimo na mifugo ina mtumishi mmoja.
Hata hivyo, alisema pamoja na watumishi hao 35 kukumbwa katika zoezi hilo hakuna huduma iliyosimama licha ya kuwepo upungufu katika baadhi ya maeneo.
Alisema katika ya watumishi hao wa afya 26 kuna waganga wa vituo, madaktari wasaidizi, matabibu na wauguzi.
Tupia Comments: