Vijana wameshauriwa kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa kuwawezasha kwa ajili ya shughuli za kijasiriamali ili kujikwamua na hali ngumu ya uchumi.
Akizungumza katika mafunzo kwa wajasiriamali Vijana Mkurugenzi Ujasiriamali Idara ya Uwezeshaji Zanzibar Zeana Hamad Kassim amesema kwamba mikopo hiyo inatolewa kwa lengo la kuwezesha vijana kuweza kujiajiri ili kupunguza tatizo la ajira Zanzibar.
Amesema serikali inafanya jitahada mbalimbali ikiwemo utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali vijana ili kupunguza idadi kubwa ya vijana wasio na ajira ambapo taarifa zinaonesha vijana wamebadilika mtazamo wa kutengemea ajira serikalini na kujikita katika ujasiriamali ili kujiwezesha kiuchumi.
Wamesema licha ya kuwa na muamko wa kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo za ujasiriamali ili kujikwamua na hali ngumu ya uchumi lakini bado wanakabiliwa na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali pamoja na ukosefu wa masoko ya kuuzia bidhaa wanazozizalisha hali inayopelekea kuvunjia moyo kwa kile wanachokifanya hivyo serikali kuliangalia kwa kina suala hili na sio kuwa wezesha tu bali hada masoko kuwatafutia kwa wakati.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoandaliwa na Jumuiya ya vijana ZAFAYCO yanalengo la kutoa hamasa kwa vijana juu ya umuhimu wa kujiajiri wenyewe katika Nyanja za maendeleo.
Tupia Comments: