Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017 wekundu wa Msimbazi Simba walisafiri hadi mjini Dodoma May 27 kucheza dhidi ya Mbao FC katika uwanja huru wa Jamhuri Dodoma kucheza mchezo wao wa fainali wa Kombe la Azam Sports Federation Cup.
Simba waliingia katika mchezo huo wakiwa na jitihada za kuhakikisha wanapata ushindi na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kutoshiriki kwa muda mrefu kutokana na kutopata nafasi ya Ubingwa wa Ligi Kuu au wa FA.
Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na wabunge mbalimbali, Simba wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Simba yakifungwa na Fredrick Blagnon dakika ya 95 baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Abdi Banda na Shiza Kichuya dakika ya 120 aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Mbao kushika.
Goli pekee la Mbao FC ambao baada ya mchezo walimzonga muamuzi limefungwa na Ndaki Robert dakika ya 109, kiungo wa Simba James Kotei raia wa Ghana ndio alikuwa mchezaji bora wa mechi kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonesha, Simba sasa itashiriki michuano ya Kombe la shirikisho msimu wa 2017/2018.
Tupia Comments: