Wizara ya elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar imesema kutokana na uharibifu mkubwa wa majengo ya skuli Unguja na Pemba uliosababishwa na mvua zinazoendelea, Serikali kwa makusudi itachukua juhudi za kuyafanyia matengenezo majengo hayo ili wanafunzi kuwa katika mazingira salama.
Akizungumza na Zanzibar24, Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Asya Iddi Issa amesema skuli nyingi unguja na pemba zinahitaji kufanyiwa matengenezo yaharaka kutokana skuli hizo kuingiliwa na maji ya mvua na kusababisha athari ikiwemo kuta za skuli kufanya nyufa, kubomoka kwa vyoo,kuvuja kwa mapaa na kuharibika kwa mazingira ya maeneo ya skuli.
Amezitaja miongoni mwa skuli za unguja zilizopata athari mbalimbali kutokana na mvua ni Kibuyuni, Zingwezingwe, Bwejuu, Kajengwa, Miwaleni, Kizimkazi mkunguni, Miwani, Mchangani, Koani, Fuoni chunga, Lumumba, Ben-bella, Kidongo chekundu, Nyerere, Jang’ombe na Muembe ladu na kutoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kutoa msaada ili kuwasaidia watoto kusoma katika mazingira bora.
Tupia Comments: