May 7, 2017 Emmanuel Macron alichaguliwa kuwa Rais mpya wa Ufaransa kuchukua nafasi ya François Hollande ambapo pamoja na habari za ushindi wake kuwa gumzo, gumzo jingine ni kupitwa kiumri na mke wake Brigitte Trogneux.
Unaambiwa Brigitte alikua ni Mwalimu wake ambaye aliwahi kumfundisha miaka 24 iliyopita ambapo wakati huo Macron alikua na umri wa miaka 15 ambapo alipokuwa na umri wa miaka 17 alimtamkia Mwalimu wake huyo kwamba siku moja atamuoa.
Ahadi ya Macron ilitimia mwaka 2007 baada ya kufunga ndoa na Brigitte Trogneaux aliyetengana na mumewe Auziere mwaka 2006, Brigitte kwa sasa ana umri wa miaka 64 akiwa na wajukuu saba huku akimzidi kwa miaka 25 Rais Macron ambaye ana miaka 39.
Tupia Comments: