Ubelgiji .Wakati mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe, Mbwana Samatta akitamba na Genk, klabu ya Standard Liege imebadilisha uhamisho wa mkopo wa wachezaji watatu wa TP Mazembe na kuwasajili kwa mkataba wa kudumu.
Samatta alinunuliwa na Genk akitokea Mazembe mwaka jana amekuwa mwenye mafanikio katika klabu yake jambo lililowavuta mabingwa wa Ubelgiji kujitosa DR Congo kuchukua nyota wengine.
Jonathan Bolingi, Merveille Bope na Christian Luyindama wote wamejihakikishia maisha katika klabu ya Standard Liege.
Nyota hao watatu walijiunga na klabu hiyo ya Ubelgiji kwa mkopo wa muda mrefu wakitokea kwa mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe, lakini sasa umekuwa uhamisho wa kudumu.
Mshambuliaji Bolingi (22), amecheza mechi 10 za timu ya taifa DR Congo 'Leopards' na amecheza michezo sita akiwa na Standard.
Kiungo mzoefu Bope (24), amecheza mechi mbili, lakini ameichezea timu ya taifa ya DR Congo mechi nane.
Beki Luyindama (23), amecheza mechi tano na mabingwa hao wa Ubelgiji na kufunga bao moja.
Tupia Comments: