Wanafunzi watatu kati ya 24 wa shule ya msingi Butwa, waliozama katika ziwa Victoria, kisiwa cha Butwa, wamefariki dunia.
Awali wanafunzi 21 waliokolewa na watatu hawakuonekana lakini saa chache baadaye, miili mitatu iliopolewa. Ajali hiyo ilitokea jana saa 10 alasiri.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema wanafunzi hao walikuwa kwenye mtumbwi waliotumia kuvuka wakitoka shuleni.
Tupia Comments: