Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Kagera, Daraja la Kemondo lililoko Barabara Kuu ya Bukoba – Mwanza, Bukoba – Dar es Salaam limekatika na kusababisha magari kushindwa kupita.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, magari yote ya abiria na mizigo yanayoenda mikoani yanalazimika kuzunguka hadi eneo la Kyetema kupitia Katerero, Kanazi, Rwagati hadi Kanyinya ndipo yatokeze mbele kidogo ya mji wa Kemondo na kuendelea na safari zake.
Mawasiliano yamekuwa ya tabu sana kwa Magari na Wasafiri wanaotumia Barabara Kuu inayounganisha Mji wa Bukoba mkoani Kagera na Maeneo jirani ya Mkoa wa Geita, Mwanza na Shinyang’a, kutokana na barabara hiyo kuu kuharibika vibaya eneo la Kemondo kama picha zinavyoelezea.
Hofu ni kwamba, barabara inayotumika sasa ni finyu na magari mengi ni makubwa yanayopita kuelekea nje ya nchi kupitia Mpaka wa Mtukula kwenda Uganda.
Mashuhuda pia wameeleza kuwa barabara inayotumika kwa sasa kupitisha magari hayo inakorongo kubwa na karavati moja hali inayoweza kusababisha barabara hiyo kukatika na kukosa pa kupita kabisa.
Tupia Comments: