Tamasha la filamu la nchi za jahazi Zanzibar (ZIFF) leo wametangaza rasmi filamu zilizo chaguliwa kuingia katika kugombania tunzo mbalimbali katika Tamasha la mwaka huu litakalofanyika kuanzia July 8 mpaka 16 ndani ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Akizungumzia uchaguzi wa filamu Mkurugenzi wa ZIFF Fabrizio Colombo amesema kuwa zoezi la kuchagua filamu lilikuwa gumu sana katika mwaka huu kutokana na wingi wa filamu, zaidi ya filamu 600 zilikuwa katika maombi ya kwenye tamasha hilo.
“Ilikua ni kazi ngumu kuchagua kutoka katika filamu nyingi zilizoletwa kwenye tamasha letu. Lakini wingi wa filamu nzuri kutoka pande zote za dunia ni dalili ya vipi tamasha la ZIFF linavyochukuliwa kuwa miongoni mwa tamasha kubwa kabisa katika bara la Africa na Dunia kwa ujumla…”
Watengenezaji wa filamu kutoka katika nchi zaidi ya 70 waliomba filamu zao kushiriki katika tamasha, kati ya hizo nchi ambazo filamu zake zimechaguliwa ni Kenya, Canada, Spain, France, South Africa, Tanzania, India, Australia, the United States, Nigeria, Rwanda, Brasil, Ghana, Chad, Uganda, Mozambique, Hungary, UK, na Ethiopia.
Filamu hizo zitashindana katika vipengele mbalimbali ikiwemo Tunzo maalum ya ZIFF ya Golden, Tunzo ya Sembene Ousmane , Best African Film, Tunzo ya Adiaha kwa mtengenezaji wa documentari wa kike, Filamu bora ya kimataifa, Filamu bora kutoka katika nchi za jahazi, Tunzo ya Emerson of Zanzibar na Tunzo ya Trace East African Music.
Tamasha la ZIFF kwa mwaka huu limetoa heshima ya kipekee kwa filamu ya Kitanzania kupata heshima ya kuoneshwa kwenye usiku wa ufunguzi. Filamu hiyo inayoitwa T-Junction imeongozwa na Amil Shivji na itaoneshwa kwa mara ya kwanza katika tamasha hili. Filamu hii imebeba sura mpya katika tasnia ya filamu ikiwahusisha waigizaji Magdalena Christopher na Hawa Ally
Tupia Comments: