Shughuli za kampeni zimekamilika nchini Ufaransa kabla ya awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais.
Siku ya mwisho ilighubikwa na mashambulizi ya Waislamu wenye itikadi kali mnamo Alhamisi.
Shambulio hilo liliwafanya baadhi ya wagombezi kuahirisha mikutano yao; lakini hata hivyo wote walishutumu kitendo hicho kilichohatarisha usalama wa kitaifa.
Kiongozi wa mashtaka wa Paris amethibitisha kuwa kijikaratasi kilichopatikana karibu na maiti ya mtu aliyefyatua risasi na kumuua polisi, kilikuwa na ujumbe wa kupongeza kundi la Islamic State.
Kiongozi huyo wa mashtaka amesema kuwa kundi lake linachunguza kugundua iwapo Karim Cheurfi alikuwa na washirika wowote.
Polisi wa Ufaransa wamewazuilia watu watatu walio na uhusiano na Chuorfi ambao wanaendelea kuwahoji.
Tupia Comments: