Raisi John Joseph Pombe Magufuli bado anaendelea na kazi yake ya kuisafisha nchi yetu ambayo haikuwa safi katika kila idara.

Nchi iliharibiwa kuanzia serikalini kwenyewe hadi katika ngazi ya mwananchi wa kawaida kiasi cha kuona kwamba rushwa ni jambo la kawaida wakati ukweli upo wazi kwamba rushwa ni aduai wa haki.

Mheshimiwa raisi Magufuli alizaliwa mwaka 1959 na sasa ana umri wa miaka 57 umri ambao katika duru za siasa na uongozi ni umri sawasawa wa kuendelea kuchapa kazi khasa ukiwa kiongozi wa nchi.

Ni dhahiri kwamba nchi sasa imeanza kunyooka si tu katika kuweka nidhamu kwenye idara za serikali bali pia katika sehemu nyingine muhimu zikiwemo idara ya mapato na vyanzo vingine vya mapato.

Tokea achaguliwe mwaka 2015 hadi sasa raisi John Magufuli amefanikisha kwa kiasi cha asilimia 100 mambo yafuatayo:

Hadi mwaka 2016

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Morocco pale kinondoni Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kupambana na Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.

Hivyo basi kwa maoni yangu ni kwamba wakati umefika sasa wa kuandaaa utaratibu wa kupigwa kwa kura ya maoni ili kuwauliza wananchi kama wanaridhia kufanyiwa mabadiliko kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kubadili kipindi cha uongozi wa raisi kutoka miaka 5 hadi miaka ishirini ikiwa ni miongo miwili ya kuijenga nchi.

Ikiwa raisi John Magufuli atapewa miaka 20 ya kuongoza nchi yetu kufika katika kule tunakokusudia kwamba anapata nafasi kwa uwazi zaidi wa kupanga mipango mingine zaidi ya maendeleo ya taifa letu.

Sasa tukiangalia na kupiga picha jinsi nchi yetu ya Tanzania itakapokuwa ifikapo mwaka 2035.

1. Umeme utakuwa umeenea nchi nzima.

Kwa kuendelea kutumia rasilimali ambazo nchi yetu inazo kama gesi serikali ya raisi Magufuli inaweza kabisa kuwezesha umeme kuwa umesamba nchi nzima ifikapo mwaka 2035.

2. Rushwa na Ufisadi vitaanza kuwa historia.

Hadi kufikia mwaka 2035 watanzania watakuwa wakielewa madhara ya kupokea na kutoa rushwa na pia kuendekeza masuala ya kifisadi.

Idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu watakuwa wamejiriwa katika sehemu mbalimbali nchini khasa katika idara kama TRA, viwanja vya ndege na bandari zetu kubwa za Dar-es-Salaaa, Tanga, Zanzibar na Mtwara.

3. Watanzania watakuwa ni wachapa kazi.

Kufikia mwaka 2035 biashara ya madawa ya kulevya na idaidi ya vijana waso na kazi itakuwa imedhibitiwa hivyo kuwepo na vijana wengi ambao ni waajiriwa katika nyanja mbalimbali. Watanzania watakuwa wakichapa kazi katika kuitikia kwa bidii kauli mbiu ya raisi Magufuli ya "Hapa Kazi Tu"

Pia watanzania watakuwa wakithamini kazi zao na kuanza kupata uwezo hata wa kujenga nyumba za kuishi na uwezo wa kupata mikopo kutpka katika mabenki mbalimbali nchini katika viwango vya riba vinavyokubalika.

4. Uchumi wa viwanda kukua pamoja na Miundombinu.

Kwa mujibu wa machapisho mbaimbali kutoka wizara ya viwanda na biashara, sera ya viwanda haijaanzishwa na serikali ya raisi Magufuli. Sera hii ilianzishwa mwaka 1996 na waziri wa wakati ule wa viwanda na biashara marehemu Dr Abdalah Kigoda ambae aliita Sustainable industrial development policy 1996-2020.

Sera hiyo ililenga katika kuhakikisha kwamba hadi kufikia mwaka 2020 Tanzania itakuwa inatumia mtaji wa ndani yaani "Domestic Capital" kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza bidhaa ndogondogo au "basic capital good industries".

Tayari leo Serikali ya awamu ya tano imewezesha kufunguliwa kwa viwanda kadhaa vya kusindika chakula, maziwa Simiyu kujengwa kwa viwanda vya kutengeza vyuma na kile cha kutengeza vigae mkoani Pwani.

Pia Miundombinu mbalimbali itapata nafasi ya kukamilishwa kwa ujenzi wake na kufikia mwaka huo wa 2035, kutakuwa na reli ya kati ya kiwango cha standard gorge na miundombinu mingine kana barabara za lami za kueleweka.

5. Viashiria vikuu vya uchumi kukua na kuimarika.

Viashiria hivyo ambavyo vimo katika maeneo ya Madini, nishati, Mawasiliano na usafirishaji vitakuwa vimeimarika kutokana na wenye makampuni kuwa wameorodhesha biashara zao katika soko la hisa ambalo litaloa fursa kwa wananchi kuweza kuwa na hisa katika makapmuni hayo na hivyo kuimarisha mzunguko wa fedha wa ndani.

Viashiria vingine kama mabenki watakuwa na uwezo wa kukopesha fedha kwa wananchi ambao wengi watakuwa ni waajiriwa katika sehemu mbalimbali.

Ni wazi kabisa sasa kwamba kero za wananchi ambazo walikuwa wakizipigia kelele zimekuwa zinatatuliwa na serikali ya awamu ya tano.

Katika nchi yoyote ile kunapotokea kiongozi ambae atajitolea kufanya usafi wa aina yake na kwa kutumia mtindo wake wa kipekee, wananchi wana budi kumuunga mkono kiongozi huyo.

Hatufahamu ikiwa wagombea wa UKAWA wangeanza na sera ya hapa kazi tu au wangekuja kivingine lakini ni wazi wananchi tuling'amua hilo na kuamua kuwapa madaraka serikali ya raisi John Magufuli.

Raisi John Magufuli bado anaendelea kupingwa jitihada zake za kuonyoosha nchi yetu na baadhi ya wale wanaompinga ni walewale walotaka mtu wa aina ya raisi John Magufuli. Ikiwa raisi Magufuli ataishia katikati na kumwachia mtu mwingine aendeleze yake aloyaanza ni wazi kuwa kila kitu kitarudi kama mwanzo nai huenda ikawa mbaya zaidi.

Mashine za Scanners zitazimwa katika viwanja vya ndege na bandarini na kuendeleza utoroshaji wa madini na nyara za serikali na pia biashara ya madawa ya kulevya itashamiri waziwazi kama ilivyokuwa mwanzo.

Fedha za umma zitaibiwa kwa safari za nje ya nchi na pia mishahara hewa itarudiwa kulipwa kwa watumishi hewa. Kuna kila dalili kwamba hali ambayo Tanzania ilikuwa nayo kabla ya kuapishwa kwa raisi John Magufuli mwezi November mwaka 2015 itarudia kama ilivyokuwa mara tu atakapomaliza uongozi wake na hiyo itakuwa ni mapema sana.

Ila ni wazi kuwa raisi John Magufuli anafaa kuendelea kuwepo kwa miongo miwili ili aweze kurekebisha kila kasoro ambazo zilikuwepo kabla ya uongozi wake na kujenga mizizi ya kuheshimu kazi na matumizi ya hekima ya fedha za umma.

Halitakuwa jambo jema kwa yeye kuishia katikati katika mipango yake ambayo inaonekana ikiwa hataimaliza basi inaweza kuishia katikati na nchi yetu isifike katika ile nchi ya ahadi ya kila mtanzania kufaidi keki ya taifa.

Ni wakati basi, wa kuibadili katika yetu kwa kuitisha kura ya maoni ili raisi John Magufuli aongezewe muda wa kuongoza Tanzania hadi mwaka 2035.

Je Mdau una maoni gani?

NB:

Jaribu kutoingiza sana siasa za vyama katika maoni yako tuangalie zaidi utendaji wa raisi John Magufuli ingawa anatoka katika chama cha CCM.

Karibu.

Maoni ya Richard/Jamii Forums

Tupia Comments: