Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini imemkamata mmiliki na kusitisha huduma za kampuni ya uzalishaji na kuhifadhi kemikali zinazotumiwa kutengeneza dawa za kulevya.
Akitoa taarifa hiyo, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Rogers Sianga amesema taarifa hiyo ni ya awali na kwamba uchunguzi unaendelea na endapo utakamilika, mmiliki huyo atafikishwa mahakamani.
Katika hatua nyingine Kamishna Sianga amesema katika ukaguzi wao wamekamata zaidi ya lita 6000 za kemikali zinazoweza kutengenezea Dawa za Kulevya huku mmiliki huyo akituhumiwa kuwa na maghala mengine katika mikoa ya Kilimanjaro na Pwani.

Tupia Comments: